Mwanamke anayejulikana kama Bhateri Devi mwenye umri wa miaka 66 aliyeishi katika ndoa yake kwa miaka 44 bila kupata mtoto amejifungua watoto 3 mapacha baada ya kufanya tiba inayojulikana kama IVF . mwanamke huyo ameshika rekodi ya kuwa wa kwanza kujifungua mapacha akiwa na umri mkubwa. Mungu amesikia kilio chake kwa kumjaliwa watoto 3 wawili wa kiume na mmoja wa kike. Mume wa mama huyo Deva Sigh 64 anasema furaha yake haina kifani, nimesubiri sana kipindi kama hiki katika maisha yangu naamini ndoto yangu itatimia ya kuwa na watoto ambao watakuwa warithi wangu. Bhateri ni mke wangu wa kwanza lakini baada ya kushindwa kupata mtoto niliamua kuoa mara mbili pia sikubahatika kupata watoto kupitia wake hao, nina furaha sana na ninaahidi kutoa matunzo mazuri kwa familia yangu
No comments:
Post a Comment