
Mwanamuziki mashuhuri kutoka Gabon Oliver Ngoma ameaga dunia. Oliver aliyezaliwa Machi 23, 1959, alishamiri sana katika muziki ya Zouk na reggae, na alisifika sana pia kwa upigaji gitaa. Aliingizwa katika fani ya muziki na baba yake ambaye pia alikuwa mwalimu wa ala mbali mbali za muziki. Oliver alijiunga na bendi ya shule Capo Sound alipokuwa akisomea taaluma ya uhasibu.Hata hivyo alionyesha mapenzi zaidi na muziki na akapewa ufadhili wa masomo ya uandishi na kupiga picha nchini Ufaransa. Mwaka 1989 Ngoma, aliyepewa jina la utani la Nolina kujizolea umaarufu zaidi kwa wimbo wake Bane,uliochezwa katika nchi zote za Afrika na ng'ambo.
No comments:
Post a Comment