Kurasa Zetu

Monday, June 28, 2010

Afukua MAITI na kufanya nayo Mapenzi

Kijana mwenye umri wa miaka 20 wa nchi ya kusini mwa Amerika ya Guyana amewashangaza watu wengi kwa kitendo chake cha kufukua maiti ya bibi wa miaka 75 na kisha kufanya nayo mapenzi. Kijana huyo aliyetajwa kwa jina la Roopram Bacchus ambaye hufanya kazi ya kuokota taka, alipandishwa kizimbani ijumaa kujibu mashtaka yanayomkabili. Bacchus alikiri mashtaka aliyofunguliwa ya kufanya mapenzi na maiti.
Kijana huyo alikiri kulifukua kaburi la bibi mwenye umri wa miaka 75 na kisha kufanya mapenzi na maiti yake. Bacchus alijitetea kuwa ana matatizo ya kupenda sana pombe ambayo ndiyo iliyompelekea akafanya kitendo hicho. Jaji aliamuru afanyiwe uchunguzi wa akili zake na alimuamuru alipe faini ya dola 200 za Kimarekani. Atatupwa jela mwaka mmoja kama akishindwa kulipa faini hiyo. Kamanda wa polisi wa eneo hilo, Steve Merai alisema kuwa Bacchus alilifukua kaburi la bibi huyo siku moja baada ya bibi huyo kuzikwa.
"Bacchus alilivunja jeneza, aliitoa maiti toka kwenye jeneza na alifanya nayo mapenzi", alisema kamanda huyo wa polisi. Kamanda huyo wa polisi aliongeza kuwa Bacchus na familia ya bibi huyo walikuwa ni majirani.

IM CRAZZY BUT IM NOT STUPID - UUUUUUUUUUUUUWIII SOMA HII

One truck driver was doing his usual delivery to IMH (Institute of mental health).
He discovered a flat tyre when he was about to go home. He jacked up the truck and took the flat tyre down. When he was about to fix the spare tyre, he accidentally dropped all the bolts into the drain.. As he can't fish the bolts out, he started to panic. One patient happened to walk past and asked the driver what happened. The driver thought to himself, since there's nothing much he can do; he told the patient the whole incident. The patient laughed at him said "can't even fix such a simple problem.... no wonder you are destined to be a truck driver..." Here's what you can do, take one bolt each from the other 3 tyres and fix it onto this tyre. Then drive to the nearest workshop and replace the missing ones, easy as that" The driver was very impressed and asked "You're so smart but why are you here at the IMH?"

Patient replied: "Hello, I stay here because I'm crazy....... not STUPID !"

Monday, June 21, 2010

Raia wa wahofia kupotea Afrika


Wasiwasi unazidi kuongezeka juu ya usalama wa wakurugenzi wa migodi ambao ni raia wa Australia kutokana na ndege yao kutokujulikana ilipo. Ndege hiyo ilikuwa ikitokea Cameroon kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Abiria tisa walikuwepo kwenye ndege hiyo, akiwemo mmoja wa matajiri wakubwa wa Australia Ken Talbot (pichani). Kundi hilo lilitoka katika mji mkuu wa Cameroon, Yaounde siku ya Jumamosi kutembelea miradi ya madini ya chuma huko Yangadou, eneo lililo kijijini huko Kongo.
Ken Talbot, tajiri mkubwa Australia, ambaye naye hajulikani alipo Jeshi la Cameroon linaongoza msako wa ardhini na angani kwenye msitu mkubwa sana. Ndege waliyokuwa wakisafiria lilikodishwa na kampuni ya migodi ya Australia, Sundance Resources. Eneo walilotembelea ni pamoja na mradi wa Mbalam linalosambaa mpaka Cameroon na Congo, ambapo Sundance Resources lina matumaini ya kupata tani milioni 35 ya madini ya chuma kwa mwaka. Shirika la habari la AFP limemnukuu waziri wa mambo ya nje wa Australia Stephen Smith akisema, " Tuna wasiwasi mkubwa juu ya usalama wao."Sundance Resources imesema baada ya kuripotiwa kuwa ndege haikutua siku ya Jumamosi jitihada zake zimelenga kusaidiana na mamlaka za Cameroon, Congo na nchi jirani ya Gabon.Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo imesema " shughuli zote zimesimamishwa, huku raslimali zote zikielekezwa kwenye jitihada za msako na uokozi."Msemaji wa ofisi ya wizara ya mambo ya nje ya Uingereza amesema wafanyakazi wa Cameroon walikuwa wanajaribu kutambua nani alikuwa kwenye ndege hiyo, baada ya mashirika ya habari kuripoti kuwa Waingereza wawili walikuwa miongoni mwa abiria hao."Tumepata taarifa hizo na tunafanya uchunguzi. Wafanyakazi wetu wa ubalozini wamekuwa wakiwasiliana na balozi ndogo ya Australia."
Mamilioni ya watu wanakosa maji ya kunywa China kutokana na hali hii ya mafuriko

Cameroon yawa ya kwanza kuaga mashindano ya Kombe la Dunia

 Camerooon imekuwa timu ya kwanza kuondolewa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini baada ya kushindwa mabao 2-1 na Denmark mjini Pretoria. Cameroon ndiyo waliotangulia kufunga katika dakika ya 10 kupitia nahodha wao Samuel Eto'o, akimalizia pasi ya Achille Webo.  Katika dakika ya 33, Nicklas Bendtner, aliisawazishia Denmark baada ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa Simon Kjaer. Bao la ushindi la Denmark lilifungwa katika dakika ya 61 na Dennis Rommedahl baada ya kumzidi kasi Jean Makoun kutokea upande wa kulia wa uwanja.  Indomitable Lions bado wana mechi moja iliyosalia dhidi ya Uholanzi ambayo tayari imekwishafuzu kwa raundi ya pili, na hata ushindi katika mechi hiyo hautaiwezesha Cameroon kusonga mbele. Nafasi ya pili ya kufuzu miongoni mwa 16 bora kutoka kundi E itang'ang'aniwa na Denmark na Japan, Alhamisi ijayo, timu hizo mbili zimekwishaifunga Cameroon. Uholanzi ilifuzu mapema Jumamosi baada ya kuifunga Japan bao 1-0.

Kondom zenye meno zazinduliwa rasmi Afrika Kusini


Kondomu mpya kwaajili ya wanawake zenye meno kwaajili ya kuwafundisha adabu wabakaji zimezinduliwa nchini Afrika Kusini. Kondomu hizo zinazoitwa "Rape-aXe" zilikuwa ni ndoto ya miaka 40 ya daktari wa nchini Afrika Kusini, Dr Sonnet Ehlers ambaye wakati akiwa na umri wa miaka 20 akisomea udaktari alikutana na mwanamke aliyebakwa ambaye alikuwa akilalamika sana. Mwanamke huyo alimuambia Ehlers "Natamani kama kungekuwa na meno huko chini, ningemfundisha adabu yule". Ehlers alisema kuwa alimwahidi mwanamke huyo kuwa siku moja atatengeneza kitu cha kuwasaidia.Katika kuthibitisha ahadi yake, Ehlers amezindua kondomu kwaajili ya wanawake zinazoitwa "Rape-Axe" ambazo zimeanza kutumika wakati huu wa kombe la dunia. Kondomu hizo zina kitu kama meno kwa ndani. Mwanamke anayeivaa kondomu hiyo anapobakwa, meno katika kondomu hiyo huunasa uume kama pingu. Kondomu hiyo inaponasa kwenye uume, huwa haitoki kirahisi na mtu anapolazimisha kuitoa ndivyo inavyozidi kuubana uume kwa meno yake. Ni madaktari pekee ndio wanaoweza kuinasua kondomu hiyo hivyo kuwawezesha madaktari kuwagundua wabakaji kirahisi na kuwaripoti polisi. "Inasababisha maumivu makali", Ehlers aliiambia televisheni ya CNN katika mahojiano na televisheni hiyo kuhusiana na kondomu hizo. "Mbakaji hataweza kukojoa wala kutembea wakati inaponasa kwenye uume wake, kama atajaribu kuitoa kwa nguvu, itaubana zaidi uume wake", alisema Ehlers. Ehlers anasambaza jumla ya kondomu 30,000 kwa wanawake nchini Afrika Kusini ili wajilinde na wabakaji wakati wa fainali za kombe la dunia zinazoendelea nchini humo.
Hata hivyo kondomu hizo zimekumbwa na malalamiko toka kwa watu ambao wanahofia kondomu hizo zinaweza kutumiwa vibaya na wanawake kuwakomesha wanaume. Mwanamke mwenye hasira kwa mpenzi wake anaweza kuzitumia kondomu hizo kumuaibisha mpenzi wake. Hatari nyingine iliyoelezwa kuhusiana na kondomu hizo ni mwanamke kushambuliwa na mwanaume mbakaji kwa hasira za maumivu atakayoyapata.
Ehlers kwa upande wake amezitetea kondomu hizo kuwa zinahitajika ili kupunguza idadi ya wanawake wanaobakwa kila siku nchini Afrika Kusini.

Ungekuwa wewe ungefanyaje?

Whether Conservative, Liberal or Labour , I think you'll get a kick out of this!

A little boy goes to his dad and asks, 'What is Politics?'
Dad says, 'Well son, let me try to explain it this way: I am the head of the family, so call me The Prime Minister. Your mother is the administrator of the money, so we call her the Government. We are here to take care of your needs, so we will call you the People. The nanny, we will consider her the Working Class. And your baby brother, we will call him the Future. Now think about that and see if it makes sense.' So the little boy goes off to bed thinking about what Dad has said. Later that night, he hears his baby brother crying, so he gets up to check on him. He finds that the baby has severely soiled his nappy. So the little boy goes to his parent's room and finds his mother asleep. not wanting to wake her, he goes to the nanny's room. Finding the door locked, he peeks in the keyhole and sees his father in bed with the nanny.. He gives up and goes back to bed. The next morning, the little boy say's to his father, 'Dad, I think I understand the concept of politics now. ' The father says, 'Good, son, tell me in your own words what you think politics is all about.' The little boy replies, 'The Prime Minister is screwing the Working Class while the government is sound asleep. The people are being ignored and the Future is in deep s**t.'

Thursday, June 17, 2010

Akili ni nywele - Baada ya maisha kumshinda uraiani avunje ukuta wa magereza ili Afungwe

Mwanaume mmoja wa nchini Msumbiji anayejulikana kwa jina la Camilo Antonia mwenye umri wa miaka 28, amevunja ukuta wa fensi ya jela na kurudi gerazani baada ya kuona maisha ya uraiani ni magumu, aliamua kurudi gerezani mwenyewe baada ya kugundua kuwa hayapendi tena maisha ya uraiani. Camilo alitumikia miaka mitano jela kati ya 10 aliyohukumiwa kwa kumuua baba yake wa kambo, alitolewa jela baada ya kupewa msamaha wa rais. Camilo ambaye alitumikia kifungo chake katika jela ya Manica iliyopo ukanda wa kati wa Msumbiji, alishindwa kustahamili maisha magumu ya uraiani na kuamua ni bora arudi jela. Alishindwa kupata kazi na alikuwa na hofu familia ya baba yake wa kambo ingejaribu kumuua. Camilo aliamua kuvunja sehemu ya ukuta wa jela ili aweze kuingia ndani. Alikamatwa na kushtakiwa kwa uharibifu wa mali za serikali na alihukumiwa kwenda jela mwaka mmoja. "Kwajinsi ninavyoona jela kwangu ni sehemu salama kuliko sehemu zote", alisema Camilo kuliambia gazeti la Noticias la nchini Msumbiji. "Sitaki kuishi jela maisha yangu yote lakini kwa wakati huu jela ni bora kuliko sehemu yoyote ile", alimalizia kusema Camilo.




Ajali mbaya Magomeni


Mmoja wa wananchi ambaye jina lake halikuweza kufahamika, akiteremka kwenye moja ya magari yaliyopata ajali eneo la Magomeni Mikumi, jijini Dar es Salaam jana.Magari hayo ni lori lenye namba za usajili T267 APE, Toyota Hiace lenye namba T189 AJG na Benz T587 AAC. Katika ajali hiyo iliyohusisha magari saba, dereva wa lori alipata majeraha na kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.

Nyerere Nje ya CCM?

Mwanafamilia ya Baba wa Taifa, Vincent Nyerere (35), pichani, wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anakusudia kuwania ubunge katika Jimbo la Musoma Mjini linaloshikiliwa na Vedatus Manyinyi wa CCM. Akizungumza na gazeti Nipashe mjini Musoma mwishoni mwa wiki iliyopita, Vincent, alisema ameamua kuwania kiti hicho ili aweze kuwasilisha mawazo na kero za wananchi wa jimbo hilo bungeni. Alieleza kuwa matatizo yanayowakabili wakazi wa jimbo hilo bado hayajatatuliwa kikamilifu likiwemo tatizo la ukosefu wa dawa hospitalini, walimu na huduma ya maji safi. “Kwa bahati nzuri wakazi wa Musoma Mjini tumezungukwa na chanzo kikubwa cha maji yaani Ziwa Victoria lakini ni asilimia ndogo sana ya wananchi wa hapa  wanaopata huduma ya majisafi…tena hali ni mbaya zaidi katika Kata ya Nyakato,” alisema. Alisema watu wengi wa manispaa hiyo wanafuata maji ziwani badala ya kuunganishiwa mabomba ili huduma hiyo ipatikane majumbani. Aidha, Vincent alisema kiwango cha elimu mkoani Mara hasa katika Manispaa ya Musoma Mjini, kimeporomoka kutokana na walimu wengi kukimbilia kwenye shule za binafsi kutokana na maslahi duni pamoja na mazingira magumu ya kazi ikiwemo nyumba za kuishi. Alifafanua kuwa kama akipata nafasi ya kuongoza jimbo hilo, atakuwa mwakilishi muadilifu wa wananchi wa Musoma Mjini huku akitaja vipaumbele vyake kuwa ni elimu na afya. Vincent Nyerere ni mtoto wa mdogo wake hayati Mwalimu Nyerere, marehemu Josephat Kiboko Nyerere ambaye alikuwa kitinda mimba katika familia ya Baba wa Taifa.

Habari chanzo: NIPASHE

Kombe la Dunia laleta simanzi Uganda

Watoto wawili wamefariki dunia nchini Uganda kutokana na moto ulioitekeza nyumba yao wakati wazazi wao walipoenda kwa jirani mwenye televisheni kuangalia kombe la dunia. Polisi mjini Kampala nchini Uganda wamesema kuwa watoto wawili wamefariki kutokana na moto ulioitekeza nyumba yao wakati wazazi wao walipoenda kuangalia mechi ya kombe la dunia.Polisi nchini Uganda wamewaonya wazazi kutowaacha watoto wao peke yao ndani ya nyumba wakati wanapoenda kuangalia mechi za kombe la dunia.
Watoto wawili wenye umri wa miaka 8 na 10 walifariki kwa moto katika wilaya ya Kayunga iliyopo magharibi mwa mji wa Kampala.Afisa wa polisi wa Kayunga, Henry Kolyanga alisema kuwa watoto hao walifariki wakati nyumba waliyokuwa wamelala iliposhika moto."Mama na Baba wa watoto hao waliacha mshumaa ukiwaka ndani ya nyumba na walienda kuangalia mechi ya kombe la dunia kwa jirani mwenye televisheni", alisema afisa huyo wa polisi."Inasemekana kuwa panya aliugonga mshumaa na mshumaa huo uliangukia kwenye meza na kukiunguza kitambaa cha mezani na kusababisha moto mkubwa ulioitekeza nyumba yote", alimalizia kusema afisa huyo wa polisi.

Ukistaajabu ya Musa utaona ya filauni ........Alazimishwa kuoa ngo'ombe baada ya kumbaka

Kijana Ngurah Alit mwenye umri wa miaka 18 alikamatwa kwenye kijiji chake cha Yeh Embang katika kisiwa cha Bali nchini Indonesia, akiwa uchi wa mnyama akifanya mapenzi na ng'ombe. Alit alijitetea kuwa ng'ombe huyo ndiye aliyemtongoza yeye na kumvutia kufanya naye mapenzi.Alit alidai kuwa aliamini kuwa ng'ombe huyo alikuwa ni msichana mrembo ambaye alikuwa akimfanyia mitego mbalimbali ili afanye naye mapenzi.Pamoja na utetezi wake, Alit alilazimishwa amuoe ng'ombe huyo na harusi ya kitamaduni iliandaliwa.
Wakati polisi wakiwaweka waandishi wa habari mbali na eneo la harusi, Alit alizimia kabla ya kukabidhiwa rasmi 'mke' wake.Hata hivyo Alit aligeuka mjane punde baada ya harusi baada ya bi harusi wake kuzamishwa kwenye bahari kama mojawapo ya imani za kijiji hicho.Ili kusafishika na kitendo chake, Alit aliogeshwa kwenye ufukwe wa bahari.Mkuu wa kijiji hicho alisema baada ya harusi hiyo kuwa kijiji sasa kimesafishika baada ya tukio hilo lililoleta aibu kwenye kijiji.

Tuesday, June 15, 2010

Mwanamke Mgumba wa miaka 66 azaa mapacha 3

Mwanamke anayejulikana kama Bhateri Devi mwenye umri wa miaka 66 aliyeishi katika ndoa yake kwa miaka 44 bila kupata mtoto amejifungua watoto 3 mapacha baada ya kufanya tiba inayojulikana kama IVF . mwanamke huyo ameshika rekodi ya kuwa wa kwanza kujifungua mapacha akiwa na umri mkubwa. Mungu amesikia kilio chake kwa kumjaliwa watoto 3 wawili wa kiume na mmoja wa kike. Mume wa mama huyo  Deva Sigh 64 anasema furaha yake haina kifani, nimesubiri sana kipindi kama hiki katika maisha yangu naamini ndoto yangu itatimia ya kuwa na watoto ambao watakuwa warithi wangu. Bhateri ni mke wangu wa kwanza lakini baada ya kushindwa kupata mtoto niliamua kuoa mara mbili pia sikubahatika kupata watoto kupitia wake hao, nina furaha sana na ninaahidi kutoa matunzo mazuri kwa familia yangu

TUCTA yatoa KIBOMU nyingine kwa Serikali

SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), limesitisha mgomo ili kusubiri nyongeza ya mshahara kwa watumishi wa umma ambopo serikali imeahidi kuuongeza na kutangazwa katika kikao cha bunge linaloendela mjini Dodoma.Mbali na hilo la kusitisha mgomo, shirikisho hilo linasubiria ongezeko hilo na kusema endapo serikali haitafikia ombi lao la sh.315,000 kwa mwezi basi wameomba angalau ifikie sh.250,000 kwa mwezi. Subirio hilo la wafanyakazi hao la kutangzwa kwa kima kipya cha mshahara wa kima cha chini kinatarajiwa kutangazwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia katika kikao cha Bunge kinachoendelea Dodoma. Wafanyakazi waliwapa serikali siku saba kutangaza mshahara mpya ambapo siku inayoishia leo na kinyum na hapo mgomo wa nchi nzima utaitishwa kama walivyopanga awali.Kaimu Katibu Mkuu wa Tucta, Bw. Sylvester Rwegasira, alisema mbele ya waandishi wa habaaari kuwa wametoa siku hizo saba kutangazwad kwa mshahara mpya ahadi iliyotolewa kwenye fhotub ya bajeti iliyotolewa wiki iliyopita

Amuua dada yake kwa kupata mimba nje ya ndoa

Mahakama nchini Jordan imemuondolea adhabu ya kifo aliyohukumiwa mwanaume aliyemuua dada yake baada ya kugundua amepata mimba kabla ya kuolewa. Mahakama imeamuru mwanaume huyo atumikie kifungo cha miaka 10 jela. Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 24 alimuua dada yake mwenye umri wa miaka 26 kwa kumchomachoma na kisu tumboni mara 15 baada ya kugundua dada yake huyo amepata ujauzito kabla ya kuolewa.Awali mahakama ya mjini Amman, Jordan iliamuru mwanaume huyo ahukumiwe adhabu ya kifo lakini jana mahakama iliamuru mwanaume huyo atumikie kifungo cha miaka 10 jela baada ya familia yake kumuombea msamaha mahakamani."Alimuua dada yake baada ya dada yake huyo kumwambia kuwa alifanya mapenzi na mwanaume ambaye alisafiri kwenda kufanya kazi nchini Saudi Arabia", alisema afisa wa mahakama ambaye hakutaka kutaja jina lake.Taarifa ya mahakama ilisema kuwa mauaji hayo yalifanyika mwaka jana katika mji wa Karak wakati huo dada yake alikuwa na mimba ya wiki nne. Kwa mujibu wa sheria za Jordan, mtu anayeua naye huuliwa lakini kwa mauaji yanayoitwa "Kulinda Heshima ya Familia" adhabu ya kifo huondolewa iwapo familia ya mwanamke aliyeuliwa itaiomba mahakama ipunguze adhabu kwa muuaji.Wanawake 15 hadi 20 huuliwa kila mwaka nchini Jordan kwa staili hiyo hiyo ya kulinda heshima za familia ingawa serikali ya Jordan inafanya jitihada ya kuiondoa tamaduni hiyo potofu.

Wednesday, June 9, 2010

Rais wa Malawi atengua adhabu ya kifungo cha miaka 14 ya wanaume waliooana


Wanaume wawili wa nchini Malawi ambao ndoa yao ilisababisha watupwe jela miaka 14 kabla ya rais wa Malawi kuingilia kati na kuamuru waachiwe huru, ndoa yao imevujika ndani ya wiki mbili baada ya kuachiwa huru. Mashoga wa malawi ambao walisamehewa adhabu yao ya kifungo cha miaka 14 jela kwa kuendeleza tabia ya Sodoma na Gomora, ndoa yao imevunjika ikiwa ni miezi sita baada ya harusi yao. Steven Monjeza, 26, na Tiwonge Chimbalanga, 20, walitiwa mbaroni mwezi disemba mwaka jana baada ya kufanya sherehe za harusi mjini Blantyre kusherehekea kuoana kwao. Kukamatwa kwao kulisababisha shinikizo kubwa kwa haki za mashoga nchini Malawi, walihukumiwa kwenda jela miaka 14 lakini rais Bingu wa Mutharika alitengua adhabu hiyo mei 29. Ndani ya wiki mbili baada ya kuachiwa huru Monjeza ametangaza kuwa uhusiano wake na "mkewe" Chimbalanga umevunjika. "Sina tena uhusiano wa kimapenzi na Tiwonge Chimbalanga, nimeangukia kwenye mapenzi na mwanamke anayeitwa Dorothy Gulo,", alisema Monjeza akiongea na shirika la habari la AFP. "Tunapanga maisha ya baadae na Dorothy", aliongeza Monjeza.
Chimbalanga kwa upande wake alisema kuwa amezisoma habari za kuvunjika kwa ndoa yake kwenye magazeti. "Sijahuzunika na chochote kuhusiana na hili", alisema Chibalanga na kuongeza "Monjeza yuko huru kumuoa yoyote ampendaye kama vile ambavyo mimi nitaolewa na mwanaume atakayekuwa kipenzi cha maisha yangu, kuna wanaume wazuri wengi kila kona, nitaendelea kuwa shoga". "Kitu ambacho ningependa mjue ni kwamba hakuna mtu aliyemlazimisha kufunga ndoa na mimi mwezi disemba mwaka jana", aliongeza Chimbalanga. Chimbalanga alisema kuwa Monjeza amekuwa akishinikizwa na ndugu zake atafute mpenzi mwanamke. Mjomba wake Monjeza, Khuliwa Dennis Monjeza,alisema kuwa atahakikisha kuwa Chimbalanga hafanyi chochote ili kumnasa tena Monjeza. Akiongea kuhusu kumrudia Chimbalanga, Monjeza alisema kuwa amejifunza kwa kipindi cha miezi mitano aliyokaa jela hivyo asingependa tena kujihusha na mahusiano ya jinsia moja.

Tuesday, June 8, 2010

Hongera CRDB kwa mchango wa Mabasi mapya ya Wanafunzi Dar!


Hatimaye Bank ya CRDB imepunguza kero ya wanafunzi wa Mkoa wa Dar es salaam kwa kutoa msaada wa mabasi makubwa 5 yenye thamani ya mil 100 kila moja. Uzinduzi wa mabasi hayo umefanywa jana Dar es Salaam na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete kwa Shirika la Usafiri la Dar es Salaam (Uda) kuhadharishwa mradi usifie mikononi mwake. Waziri Mkuu alitangaza kwamba Serikali iko tayari kuwaondolea ushuru watu binafsi, kampuni na mashirika watakaoguswa na kununua mabasi kwa ajili ya mradi huo uliokabidhiwa Uda kwa mkataba na utaratibu maalumu wa uendeshaji. “Hatutakubali kuona mradi uliozinduliwa leo ukifa au ukapotea kimaajabu tu,” alisema Pinda. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uda, Martin Milanzi, magari hayo yatatoa huduma kwa njia za Kariakoo-Tegeta, Chanika-Kariakoo na Kariakoo-Mbezi Shamba kwa nauli ya Sh 100 kwa mwanafunzi. Takwimu zilizowahi kutolewa zinaonesha Dar es Salaam yenye wanafunzi zaidi ya 500 inahitaji zaidi ya mabasi 10,000 ya kawaida, kubeba idadi hiyo ya wanafunzi kila siku asubuhi wanapokwenda shuleni na jioni wanaporudi. Mh Pinda alisema “Tujitahidi kuonesha watoto kuwa tunabuni mambo yanayowezekana. Kampuni mbalimbali zione jambo hili ni letu sote. Basi moja ni Sh milioni 100 na ushuru, bila ushuru ni Sh milioni 75. Hili la kuondoa ushuru mabasi yapatikane linawezekana,” alisema Pinda na kumwelekeza Mkuu wa Mkoa, William Lukuvi, wakae kuangalia namna ya kutoa msukumo kwa wengine kuchangia.

Afrika Kusini yafukuza 'wahuni' wa Argentina

Polisi Afrika Kusini Afrika Kusini imewafukuza wanaodhaniwa kuwa mashabiki wahuni 10 kutoka Argentina ambao polisi wanasema walikuwa na mpango wa kuvuruga Kombe la Dunia. Watu hao, ambao ni miongoni mwa kundi la mashabiki 80, walikamatwa katika uwanja wa ndege wa Johannesburg na kugundulika kuwa walikuwa katika orodha ya watu waliopigwa marukuku kuingia Afrika Kusini. Polisi nchini humo wamesema hatua hiyo inaonyesha jinsi gani maandalizi ya usalama kabla ya mashindano hayo yanavyotekelezwa. Kombe la Dunia, linalofanyika barani Afrika kwa mara ya kwanza-linaanza Ijumaa. Watu hao wanasemekena kuwa wanachama wa "barras bravas" wa Argentina, makundi yanayojulikana kwa kufanya ghasia katika mashindano ya soka. Walikamatwa siku ya Jumapili baada ya kusafiri kutoka Argentina kupitia mji wa Luanda nchini Angola, na kuondoshwa Jumatatu. Kutokana na polisi, takriban wawili miongoni mwao walikuwa viongozi wa makundi hayo, na mwengine alikuwa nje kwa dhamana kutokana na makosa ya mauaji.

Mungu mlaze mahali pema peponi Oliver Ngoma

Mwanamuziki mashuhuri kutoka Gabon Oliver Ngoma ameaga dunia. Oliver aliyezaliwa Machi 23, 1959, alishamiri sana katika muziki ya Zouk na reggae, na alisifika sana pia kwa upigaji gitaa. Aliingizwa katika fani ya muziki na baba yake ambaye pia alikuwa mwalimu wa ala mbali mbali za muziki. Oliver alijiunga na bendi ya shule Capo Sound alipokuwa akisomea taaluma ya uhasibu.Hata hivyo alionyesha mapenzi zaidi na muziki na akapewa ufadhili wa masomo ya uandishi na kupiga picha nchini Ufaransa. Mwaka 1989 Ngoma, aliyepewa jina la utani la Nolina kujizolea umaarufu zaidi kwa wimbo wake Bane,uliochezwa katika nchi zote za Afrika na ng'ambo.

Viwanja vitavyotumika na mchakato wa Kombe la Dunia 2010


Jina : Mbombela Stadium
Eneo: Nelspruit
Uwezo wa kubeba watu : 46,000
Sifa : Lina jina la Asili la kiswati  “Mbombela” likiwa na maana “many people together in a small space.”  pia upo karibu na game parks

Jina : Nelson Mandela Bay Stadium.  
Eneo : Nelson Mandela Bay/Port Elizabeth 
Uwezo wa kubeba watu : 46,000 Sifa : Una jina la Mtu Maarufu Barani Afrika

 
Jina la Uwanja : Soccer City Stadium
Eneo : Johannesburg
Uwezo wa kubeba watu : 94,500
Sifa:  Uwanja utaotumika kwa mechi ya Ufunguzi na Fainal za kombe la Dunia

Jina : Green Point Stadium
Mji : Cape Town
Uwezo wa kubeba watu: 70,000
Sifa :Upo karibu na Bahari na milima ya Cape Town , unakadiriwa kujengewa na paa lenye uzito wa tani 4,500 la vioo.